
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 28, 2022, Kamanda wa Kanda hiyo Jumanne Muliro amesema vijana wengi waliokamatwa umri wao unaanzia miaka 13 hadi 21.
Amesema baada ya kuhojiwa, vijana hao wamekiri kuhusika na matukio hayo na wamendelea kuisaidia Polisi kuhakikisha wenzao wanaotoka maeneo mbalimbali waliohusika na matukio hayo wanakamatwa.
“Vijana hao wamekuwa wakitumia mapanga kuwajeruhi watu na Jeshi la Polisi tuliongea na wenyeviti wa mtaa na mabalozi tumekubaliana hali hiyo haiwezi kuendelea lazima watapambana na mkono wa chuma vijana wanaojihusisha na matukio hayoa” amesema
Amesema mbali na vijana hao kuiba mali za watu katika tukio hilo la Chanika waliwajeruhi watu 23 kwa kuwakata mapanga sehemu mbalimbali na wengi wao wapo hospitali wakiendelea na matibabu.
“vijana hao ni wadogo wamekamatwa na wameongea mambo mengi naamini kulingana na uchunguzi tunaendelea kuufanya tutafika pazuri,”amesema
Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa kupitia operesheni iliyoanza kufanyika Aprili Mosi mwaka huu hadi jana ambapo wamemhojiwa kwa kina na kukiri kutekeleza tukio hilo pamoja na wenzake wawili.
”Aprili 16 mwaka huu eneo la Mlandege Kigamboni walimkodi kijana huyo wakiwa safarini walimpiga na kitu kizito na kupoteza maisha na kufanikiwa kupora pikipiki yake na kuondoka nayo hadi maeneo ya Rufiji walikokamatwa na Polisi,”amesema
Mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake wawili walikiri Agosti 27 mwaka jana walimkodi kijana mwingine kwenye maeneo hayo ambaye alikuwa hafahamiki alipo hadi wanakamatwa.
“Lakini baada ya kuwakamata wamekiri kuhusika na tukio hilo la kumkodi kijana huyo na kumuua na kwenda kumutupa maeneo hayo hayo ya Kigamboni,”amesema
Watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa walionesha hadi sehemu ilipo pikipiki ya marehemu aliyeuawa Agosti 27 mwaka jana na kwenda kuonesha walipoenda kutupa mwili wake.
“Tulipofika pale tuliona mifupa na fuvu linalodhaniwa kuwa la binadamu hata hivyo uchunguzi bado unaendelea na ukikamilika watuhumiwa watafikishwa kwenye vyombo vya dola,”amesema