TEZI DUME NI NINI?
• Tezi dume ni moja ya tezi la uzazi la kiume ambalo kila mwanaume analo, tezi hili lipo chini ya kibofu cha mkojo na linazunguka njia ya mkojo toka kwenye kibofu kwenda kwenye uume.
• Jinsi umri unavyoongezeka tezi dume nalo huongezeka ukubwa ambao unaweza kuwa wa kawaida au saratani.
Kuna aina tatu za magonjwa ya tezi dume.
• Maambukizi ya Bakteria (Prostatitis).
• Kukua kwa tezi dume ambalo sio saratani (Benign Prostatic Hypertrophy-BPH).
• Saratani ya tezi dume.
KAZI YA TEZI DUME
• Kutoa majimaji anayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) kutengeneza manii (semen).
SARATANI YA TEZI DUME
• Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vitokanavyo na saratani kwa wanaume duniani.
• Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.
VITU VINAVYOSABABISHA SARATANI YA TEZI DUME
Chanzo hasa cha saratani ya tezi dume hakijulikani, saratani hii ina uhusiano mkubwa na;
• Umri, Wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea wanapata zaidi saratani ya tezi dume.
• Vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta, hasa ya wanyama.
• Historia ya tatizo hili kwenye familia (Genetic).
• Kuwa na uzito uliokithiri.
DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME
• Katika hatua za awali, dalili hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume lisilokuwa saratani (BPH).
Dalili hizo ni pamoja na;
• Kusikia kupata haja ndogo mara kwa mara hasa nyakati za usiku
• Haja ndogo kuchelewa kutoka
unapoanza kukojoa.
• Kutoa mkojo wenye mtiririko dhaifu na kuchuruzika kidogo kidogo baada ya kumaliza kukojoa.
• Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote.
• Kutoa mkojo au manii yaliyochanganyika na damu
• Maumivu makali sehemu mbalimbali za mwili kama saratani
imesambaa.
• Kupunguauzito, kuhisikichefuchefu,
uchovu na kizunguzungu.