ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, May 22, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Wabunge 2 mbaroni kwa kupiga mawe helkopta ya Odinga

I am Krantz by I am Krantz
Apr 4, 2022
in HABARI
0
Wabunge 2 mbaroni kwa kupiga mawe helkopta ya Odinga
0
SHARES
32
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

WABUNGE wawili kutoka nchini Kenya wanatarajiwa kuhojiwa na Ofisi ya Mlelezi wa Makosa ya Jinai kutokana na tuhuma za kuipiga mawe helkopta ya Mgombea urais nchini humo kutoka ODM, Raila Odinga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kenya … (endelea).

Wabunge hao Caleb Kositany kutoka Soy na mwenzake wa Kapseret, Oscar Sudi wameeleza kukubali wito wa polisi na kujiwasilisha kwa Ofisi za DCI za Nakuru nchini humo kwa ajili ya kuhojiwa leo tarehe 3 Aprili, 2022.

RelatedPosts

No Content Available
Load More

Aidha, imeelezwa kuwa Spika wa Kaunti ya Uasin Gishu, David Kiplagat naye alikuwa katika afisi za DCI leo asubuhi kuhojiwa kuhusu tukio hilo.

ADVERTISEMENT

Tukio hilo lilitokea tarehe 1 Aprili mwaka huu katika mazishi ya Mzee Jackson Kibori ambapo Odinga alikwenda kushiriki mazishi hayo yaliyofayika katika shamba la Samitui kaunti ya Uasin Gishu.

Inaelezwa kuwa kulitokea kundi la vijana waliopiga mawe helkopta hiyo ya Rais na kuharibu mifumo ya hewa sambamba na kuvunja vioo vya gari lake.

Aidha, baada ya tukio hilo, mpizani wa Raila katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyka Agosti mwaka huu, Naibu Rais William Ruto alilaani uhalifu huo na kuagiza vyombo vya usalama kuwachukulia hatua wote walioshiriki.

Aidha, wabunge hao ambao wanatajwa kuwa na ukaribu na Ruto wamekanusha kuhusima katika vurugu hizo.

Walisema kuwa wako tayari kuandika taarifa kwa ofisi za DCI ili kuthibitisha hawakuhusika na kisa hicho.

“Tuko tayari kubeba mzigo huo, tupo kwa ajili ya haki, tunahubiri amani siku zote, tunaelekea Nakuru kwenda kusikiliza upuuzi huu, ni upuuzi mtupu, chochote wanachotaka kufanya tuko tayari kwa hilo.

“Kama wanasiasa, tunapaswa kuacha kuajiri wahuni ili kuwasumbua wengine hata kwenye mazishi. Sio Waafrika,” wamesema.

Aidha, wamedai kushangazwa na hatua ya kuhojiwa kwao ilihali vijana waliihusika wanafahamika.

Mmoja wa wabunge hao alidai kuwa aliambatana na Raila saa chache kabla ya mazishi ya Mzee Kibor.

Related

Tags: Kenya
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 6, 2022 / BEI YA PETROLI KILIO KILA KONA / WABUNGE WACHARUKA KUPAA BEI YA MAFUTA / MAKAMBA AMALIZA UTATA BEI YA MAFUTA
HABARI

BUNDI ATUA NCCR – MAGEUZI / TUNDU LISSU, LEMA WACHOKA MAISHA YA UGHAIBUNI / MAGAZETI YA LEO MEI 22, 2022

by Shabani Rapwi
May 21, 2022
TUMEUMIZWA NA MATOKEO YA JANA – AHMED ALLY
HABARI

AFRIKA NZIMA ITAKAA KWENYE TV KUANGALIA SIMBA IKICHEZA FAINALI MICHUANO YA AFRIKA – AHMED ALLY

by Shabani Rapwi
May 21, 2022
MADHARA YA KUPAKA MATE UKENI WAKATI WA TENDO LA NDOA
HABARI

MADHARA YA KUPAKA MATE UKENI WAKATI WA TENDO LA NDOA

by Shabani Rapwi
May 21, 2022
JAMES MBATIA ASIMAMISHWA NCCR-MAGEUZI
HABARI

JAMES MBATIA ASIMAMISHWA NCCR-MAGEUZI

by Shabani Rapwi
May 21, 2022
ALIYOFANYA MIQUISSON, SAKHO AMESHINDWA KUFANYA
HABARI

ALIYOFANYA MIQUISSON, SAKHO AMESHINDWA KUFANYA

by Shabani Rapwi
May 21, 2022
BOCCO ANASTAILI HESHIMA KATIKA SOKA LA TANZANIA
HABARI

BOCCO ANASTAILI HESHIMA KATIKA SOKA LA TANZANIA

by Shabani Rapwi
May 21, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In