Iko hivi, sijui nani kakudanganya ila unatakiwa kujua kitu hiki. Katika TV kunakua na ratiba ya vipindi, kuanzia asubuhi mpaka jioni unajua kabisa kila alhamisi kuna kipindi flani na flani!
Siku ikibadilika unashangaa na unauliza “Kuna nini leo, mbona hawaonyeshi tamthilia flani?”
Sasa Dada zangu, wanaume sio kama TV. Mwanaume wako kakuzoesha, kila siku asubuhi anakupigia simu kukusalimia, mchana anakutumia meseji, jioni lazima muongee kabla ya kulalaa!
Hayo ni mazoea, sio lazima afanye hivi kila siku. Shida yako nikua, siku akiacha kukupigia simu kutwa nzima, nawe unakaa kimya, unasubiria, kesho yake uanaanza kulalamika.
“Mbona jana hujanipigia!” Tena heri hata ungeishia kulalamika tu, hapana, na mnuno juu! Haiishii hapo unaanza kuchunguza kama ana mwanamke mwingine!
Moja haikai mbili haisimami, unaanza kushika simu yake, kuangalia alikua anaongea na nani? Kumuuliza mbona umebaidlika, na mambo kibao. Mwanaume kabadilika wiki mbili tu ushaanza “Kama vipi bora tuachane!”
Labda nikupe siri moja ambayo ulikua hujiui “Mwanaume ni binadamu!” kuna wakati ana mambo yake mwenyewe, ana vitu vinamsumbua! Anataka kuwaza bila kusumbuliwa!
Najua uansema “Kama ana kitu si aniambie, mimi si ni mpenzi wake?” Dada wanaume sio kama wanawake!
Wewe ukiwa na kitu utataka kumuambia kila mtu, akusaidie au akushauri, wakati mwingine hata akusikilize tu! Sisi wanaume tunapenda kutatua changamoto zetu wenyewe.
Kama nina tatizo, nilimalize ndiyo nimuambie mke wangu “Kulikua na moja mbili tatu!” Najua ndiyo maana tunakufa mapema, ila ndiyo tulivyo.
Kwahiyo Dada, mwanaume akibadilika wiki mbili tatu acha kukimbilia kuachana na kuhisi ana mtu mwingine, wengine wana mambo yao tu amabayo wana dili nayo!
NB: Kama uko katika hali hii basi” Acha kujipa ma presha mengi na kupaniki.
Nirahisi kutengeneza Mahusiano uliyonayo kuliko kuanzisha mengine mapya.
MWISHO