
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Aprili 28, 2022 katika Kitongoji cha Mijuni Kata ya Sange wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje (DC), Anna Gidarya amethibitisha tukio hilo na kwamba Serikali inaendelea kufuatilia.
Watu walioshuhudia wamesema waliofariki ni mume, mkewe ambaye alikuwa mjamzito pamoja na mtoto wao.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Sange, Elina Mbwilla amewataja waliofariki kuwa ni Lazaro Shibanda (25), Rozalia Kijalo (22) na mtoto Ayubu Shibanda mwenye umri wa miaka minne.
Amesema wananchi walikusanyika alfajiri na kufukua udongo na hatimaye kuwakuta wakiwa wamefariki.