Katika kipindi cha miezi miwili ya February na March mwaka huu Watoto wa kike 200 wa Shule za Msingi na 28 wa Shule za Sekondari Mkoani Kigoma wamelazimika Kuacha masomo baada ya kupata mimba wakiwa Shuleni.
Kaimu Afisa Elimu Kigoma David Mwamalasi ameyasema hayo katika uzinduzi wa mashindano ya insha kitaifa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi, mradi utakaotekelezwa na Shirika la World Vision Katika Mikoa 12 Tanzania Bara wenye lengo la Kupinga vitendo vya mimba na ndoa za utotoni Mashuleni.
Katika kipindi cha mwaka 2021 Watoto wa kike 6000 wa Shule za Msingi na 600 wa Sekondari waliripotiwa kuwa Watoro kwasababu mbalimbali ikiwemo mimba, kuolewa na nyinginezo .
Mwamalasi anasema changamoto hizo zimekuwa zikichagizwa na hali ya duni ya maisha na umbali wa miundombinu ya Shule Katika baadhi ya maeneo Mkoani Kigoma.