Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewasimamisha kazi watumishi wanne wa wizara hiyo kufuatia kusuasua kwa ujenzi wa bwawa la Kwankambala wilayani Handeni mkoani Tanga.
Waziri Aweso ametangaza uamuzi huo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya maji wa wilaya ya Handeni.
Watumishi waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Hamisi Matungulu ambaye ni Msimamizi wa mradi huo kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazimgira Vijijini ( RUWASA) makao makuu, Jimmy Mwanyakunga – Mhasibu Mkuu RUWASA.