Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa ameridhia Utaratibu Uliowekwa wa Bajaj na Bodaboda kuishia kwenye Vituo Maalum Vilivyopangwa kulingana Makubaliano yaliyofikiwa Baada ya Majadiliano ya Pande zinazohusika.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa Amos Makalla alipokuwa akizungumza na Waendesha Bajaj ambao ni Walemavu walioandama hadi Ofisi kwake.
Makalla amesema hakuna Katazo la Bodaboda kuingia mjini isipokuwa kumetengwa Vituo takribani 9 vya kushushia Abiria.