Muigizaji na mshindi wa tuzo za Oscar, Will Smith amekuwa haonekani hadharani tangu tukio la kumzaba kofi mchekeshaji Chris Rock wakati wa tuzo za Oscar.
–
Nyota huyo wa The After Earth ameonekana kwa mara ya kwanza baada ya tukio hilo akiwasili katika uwanja binafsi wa ndege mjini Mumbai India.
–
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za vyombo vya habari, Smith yuko katika nchi hiyo ya Asia kutafuta msaada wa kiroho kutoka kwa gwiji wa kiroho Sadhguru.
–
Safari hiyo ya Asia ndio safari ya kwanza muigizaji huyo kuonekana waziwazi tangu tukio la tuzo za Oscar na inaelezwa muigizaji huyo yupo India kwa kupata msaada wa kiroho, kufanya mazoezi ya yoga na kutafakari.