Polisi katika Jimbo la Indiana nchini Marekani bado wanahangaika kumtambua mtoto wa kiume aliyekutwa mwezi uliopita akiwa amekufa ndani ya sanduku lililokuwa limeachwa katika eneo lililojaa miti na mbao.
–
Polisi hao wameendelea kuomba msaada wa wananchi katika kumtambua mtoto huyo ambaye ameelezewa kuwa ni mweusi na mwenye umri kati ya miaka 5 na 8.
–
Uchunguzi wa awali katika mwili wa mtoto huyo haukutoa majibu yoyote ya kuweza kusaidia kumtambua. Hata hivyo polisi bado wana matumaini kuwa ripoti moja inayosubiriwa inaweza saidia kupata taarifa muhimu ambazo zinaweza zikawaongoza kumtambua mtoto huyo.