Watu 19 wamejeruhiwa baada ya basi la Super Feo kupata ajali leo Jumapili 22 May Wilayani Tunduru likitokea Songea kwenda Dar es salaam.
ADVERTISEMENT
–
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amesema ajali hiyo imetokea Kijiji cha Huria Kata ya Namwinyu Wilaya ya Tunduru “Majeruhi 14 wametibiwa na kuruhusiwa kuondoka, majeruhi watano wanaendelea na matibabu na mmoja anategemewa kupewa rufaa kwa matibabu ya juu zaidi. Chanzo cha ajali ni mwendokasi uliopitiliza katika maeneo yenye kona nyingi na kali” DC Mtatiro.
ADVERTISEMENT