Ameandika Ahmed Ally, Meneja wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba :
“Siku moja Afrika nzima itakaa kwenye TV kuangalia Simba Sports Club ikicheza Fainali ya michuano ya Afrika. Haya ni malengo ambayo tunaishi nayo na tuko mbioni kuyatimiza Insha Allah
Miaka mitatu ya robo fainali tumejifunza mengi na tunaendelea kujifunza hasa kwenye uwekezaji wa wachezaji bora, Utawala madhubuti na mipango imara
Kucheza fainali na hata kuchukua Ubingwa wa Afrika inawezekana endapo maeneo hayo yataimarishwa. Wana Simba wenzangu tuendelee kushikamana siku yetu ya kucheza Fainali ya Afrika haiko mbali
Sisi sio timu ya kuwaza mambo madogo na kuridhika mafanikio kidogo ya ndani. Simba tulipo sasa kumfunga Mbeya Kwanza ni maisha ya kawaida sio mafanikio, mafanikio ni kuzifunga timu zilizocheza Fainali ya Afrika na kuwatoa mashindanoni. NAWAKUMBUSHA TENA BERKANE AMECHUKUA UBINGWA MSIMU HUU HAJASHINDA HATA MECHI UGENINI ZAIDI YA FAINALI. Hongereni @rsbfootball