Kiongozi wa dini ya Kiislamu ameiomba mahakama ya Kenya kutomwachilia huru licha ya kuachiliwa kwa makosa ya ugaidi.
–
Sheikh Guyo Gorsa Buru alikamatwa Januari 2018 kaskazini mwa Kenya na kushtakiwa kwa kuwa na nyenzo za kulitangaza kundi la kigaidi na kwa kushirikiana na kundi la wanamgambo wa al-Shabab.
–
Lakini wiki hii, mahakama ilimwachilia ikisema kuwa serikali imeshindwa kuthibitisha kesi yake.
–
Hata hivyo alikataa kuondoka katika gereza maarufu la Kamiti akisema anahofia maisha yake huku akidai kuwa anaweza kutekwa nyara na kuuawa na serikali mara tu atakapokuwa huru.