Basi la Kampuni ya Mohammed Clasic lililokuwa likitoka Mkoani Arusha kuelekea Kigoma limegongana uso kwa uso na fuso katika kijiji cha Ming’enyi Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara na kusababisha vifo vya Watu watatu na majeruhi 26.
–
RPC Manyara, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema fuso lilikuwa limetoka mkoani Tabora kuelekea Kilimanjaro likiwa limebeba mchele “Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kutokuzingatia alama za barabarani”
–
“Waliofariki ni Msaidizi wa dereva wa fuso, Msaidizi wa dereva wa basi pamoja na utingo wake, dereva wa basi ametoroka kusikojulikana tunaendelea kumtafuta kwa kusababisha ajali na kugharimu maisha ya Watu na majeruhi na hatua kali zitachukuliwa”
–
“Majeruhi ni Wanaume 14, Wanawake 10 na Watoto wawili ambao wote wapo katika Hospitali ya Tumaini Kateshi”