ADVERTISEMENT
Ameandika : Moud Mtanzania, shabiki wa klabu ya Simba SC
Kama Kuna mchezaji anaependwa Simba kwa sasa na ni kipenzi cha Mashabiki Basi Ni Sakho, Kwenye kundi la Mashabiki wa Simba wapatao 10 ukiwauliza Ni mchezaji gani unaempenda kwa Sasa Basi tegemea 7 watakwambia Pape Ousmane Sakho .
–
Ndio, Huyu Ni Pape Sakho Raia wa Senegal ambae usajili wake ulizungumziwa zaidi Africa na nchini kwao kutokana na kipaji chake wengi walitegemeaa angeenda ulaya lakini Ushawishi wa viongozi wa Simba waliweza kuinyaka Saini ya huyu mtoto Simba wa Teranga.
–
Ndio huyu huyu Sakho ambae kipindi anakuja Simba Mashabiki wengi tulikuwa na Imani nae kwakusema tumepata mbadala wa Louis Miquissoine (Konde Boy), Tusidanganyane kiubora Sakho tunaweza kusema Ni Bora kuliko Miquissoine lakini kwa aliyoyafanya Konde boy Sakho ameshindwa kufikia hata robo yake.
–
Sakho alipopata majeraha tulimtetea kwakusema labda akipona atauwasha Moto na kumpata huyo new Konde lakini matokeo yake Ni kumkumbuka tu kwa Miquissoine na upo mpango wakumrudisha Simba,
Kama ningekuwa Sakho ningejipa muda wa maswali na majibu :- ningejiuliza Kama nilisajiliwa mbadala wa Miquissoine Leo hii anakumbukwa na kutaka kumrudisha ” inamaana Mimi nimeshindwa kuwashawishi? Au nimeshindwa kufikia ubora wa Miquissoine? Majibu angebaki nayo mwenyewe.
–
Ukweli Ni huu Sakho Ni mchezaji mzuri sana Ila kinachomfelisha Ni kucheza na Jukwaa hii ndio Tofauti yake na Miquissoine, miq Alikuwa fighter kweli katika dakika 90 za mechi huwezi kumuona akinyanyua macho yake nakuangalia majukwaa Kama mashabiki wananishangilia , Miquissoine alikaba , alifunga Sana, Kapigwa Sana kadi za njano lakini mwiso wa siku Mashabiki tulimpenda Sana na mpaka leo tunampenda kwasababu tu Ile fighting spirit yake ilivyokuwa high kwenye kututafutia matokeo.
–
Nikweli kila mchezji ana style yake ya kiuchezaji Ila utukumbuke nasisi Mashabiki tunapenda zaidi matokeo kuliko kutushangilisha kwa kukimbia na mpira muda mwingi halafu hakuna madhara UNATUZULUMU, najuwa unanijengea mazingira yako binafsi ya You Tube ili ujitangaze lakini sisi tunakuomba uifikirie zaidi Simba zile mbwembwe punguza UNATUZULUMU.
–
By the way Huu Msimu ndio unaisha Bado unayonafasi yakutuonesha nikwanini wasenegal walichukia maamuzi ya wewe kuja Simba na kwanini usingeenda Ulaya, Bado unayonafasi yakutengeneza ufalme wako Kama ilivyokuwa kwa kibaden, Pawasa, Okwi, Chama, hata Miquissoine. TUNAKUPENDA LAKINI UNATUDHULUMU 

Ni Hayo Tu. #MoudSijambo
ADVERTISEMENT