Taarifa imetolewa na Uongozi wa Taliban ya kwamba Watangazaji wote wa kike katika vituo vya runinga Nchini Afghanistan wanatakiwa kuziba nyuso zao wanapokuwa wakitangaza.
–
Vyombo vya Habari vimekiri kupokea maagizo hayo kutoka katika Wizara ya Maadili na wamesema wanachotakiwa ni kutekeleza bila kuwa na mazungumzo wala kuuliza chochote kuhusu hatua hiyo.
ADVERTISEMENT
–
Waziri wa Habari wa Afghanistan, Akif Sadiq amekiri kuwa maagizo hayo ni maalum kwa vituo vyote vya ndani, japokuwa agizo hilo limepingwa na Watetezi wa Haki za Wanawake wa ndani na nje ya Taifa hilo.
ADVERTISEMENT