Kampuni ya Apple imesema itasitisha utengenezaji wa iPod na hivyo kumaliza kabisa safu ya bidhaa ambayo ilisaidia kuanzisha enzi mpya katika tasnia ya muziki pamoja na kampuni kubwa ya teknolojia.
–
Apple (AAPL) imesema wateja wanaweza kuendelea kununua kifaa cha iPod Touch, Kampuni hiyo imesema kwa sasa wateja wake wanaweza kusikiliza nyimbo wanazozipenda kutoka kwenye vifaa vingine vya Apple, pamoja na iPhone, iPad na Apple Watch.
–
“Muziki daima umekuwa sehemu ya msingi kwetu kama Apple, na kuileta kwa mamia ya mamilioni ya watumiaji kwa jinsi iPod ilivyoathiri zaidi tasnia ya muziki tu, pia ilifafanua upya jinsi muziki unavyogunduliwa, kusikilizwa na kushirikiwa,”
–
Ipod ilianzishwa kwa mara ya kwanza na mwanzilishi mwenza wa Apple na Mkurugenzi Mtendaji wa wakati huo Steve Jobs mwaka 2001 na ilisaidia kuiletea mafanikio makubwa Apple kwa kuwa kifaa hichi kilivutia wateja kwa uwezo wake wa kuhifadhi hadi nyimbo 1,000 kwa ubora wa zaidi ya CD enzi hizo, kwenye kifaa unachoweza kukibeba mfukoni mwako, hadi katikati ya 2007, zaidi ya vifaa milioni 100 vya iPod vilikuwa vimeuzwa.
01:22