Binti mmoja anayefahamika kwa jina la Happiness Mdoshi (15) mwanafunzi wa kidato Cha pili katika Shule ya sekondari Nyanza iliyopo mjini Geita ameshindwa kufanya mitihani yake ya Mkoa (Moco) baada ya kumwagiwa Maji ya Moto kwenye sehemu za mgongo na makalio na wenzie wakati wakisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
–
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (ACP), Henry Mwaibambe amethibisha tukio hilo Mei 19 ,2022. Kamanda Mwaibambe amesema tukio lilitokea nyumbani kwao katika mtaa wa Mkoani, Mjini Geita anapoishi happiness na bibi yake.
–
Kamanda alisema Happines alimwagiwa maji ya moto kwa bahati mbaya na mtoto mwenzie anayefahamika kwa jina la Silias Elias (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne. Baada ya kutokea kwa tukio hilo Kamanda Mwaibambe ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kuongeza umakini pindi wanapowafanyia watoto wao sherehe ili kuepukana na majanga yanayoweza kuepukika.
–
Kwa upande wake Bibi wa Happines alieleza alikuwa hafahamu kama tukio hilo litapelekea madhara kwa mjukuu wake. Alisema alichokuwa anafahamu yeye ni mjukuu wake yupo na wenzake wanafurahia siku yake ya kuzaliwa kwa bahati mbaya ikatokea mwenzie amemwagia maji ya Moto bila kujua.