ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, March 28, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKIVUA SAMAKI

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
May 23, 2022
in HABARI
0
AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKIVUA SAMAKI
0
SHARES
200
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Mei 23,2022

 

 

RelatedPosts

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

Mar 28, 2023

MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

Mar 28, 2023

TAIFA STARS YAAHIDI KUENDELEZA ILIPOISHIA

Mar 28, 2023
Load More

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Hamis Mayunga (27) mkazi wa Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ameuawa kwa kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Sam Security aitwaye Emmanuel Chacha katika eneo la Mgodi wa Almasi wa El – Hilal wilayani Kishapu.

 

–

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Mei 23,2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Mei 20,2022 majira ya saa nne usiku katika eneo la mgodi wa El – Hilal.

–

 

“Hamis Mayunga (27) mkazi wa kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu aliuawa kwa kupigwa risasi na Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Sam Security yenye makao Makuu yake Mjini Shinyanga katika eneo la Mgodi wa El Hilal.

ADVERTISEMENT

 

Huyu Hamisi Mayunga akiwa na wenzake wasiopungua 10 walikuwa wanavua samaki katika bwawa lililopo katika mgodi wa El – Hilal ndipo Mlinzi wa Kampuni ya Sam Security aitwaye Emmanuel Chacha akiwa na wenzake wanne waliondoka katika lindo lao walilopangiwa wakaenda katika bwawa hilo (ambalo siyo eneo lao la kazi, hawa hawafanyi doria) wakawazuia kuvua samaki , pakatokea kutoelewana ndipo akamfyatulia risasi kwa kututmia bunduki aina ya Shortgun ikampiga kwenye moyo upande wa kushoto na kusababisha kifo chake papo hapo”,ameeleza Kamanda Kyando.

 

–

“Mtuhumiwa wa mauaji Emmanuel Chacha alitoroka baada ya kutekeleza mauaji hayo na kutelekeza bunduki kwenye mlango wa mgodi. Tayari tunawashikilia walinzi wanne huku tukiendelea kumtafuta mtuhumiwa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake”,ameongeza Kamanda Kyando.

ADVERTISEMENT

–

 

“Natoa wito kwa walinzi wa makampuni binafsi ya ulinzi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuacha kutumia nguvu kupita kiasi…Haiwezekani mtu anavua tu samaki, vipelege umpige risasi. Nimepanga kukutana na Makampuni binafsi ya ulinzi kwani hili sasa ni tukio la pili mwezi huu ambapo hata kule Mwakitolyo Mlinzi wa Kampuni ya Light Ndovu Security Abdul Chacha naye aliua mwananchi aliyekuwa anagombana na mke wake…Yaani mtu agombane tu na mkewe umpige risasi?” amesema Kamanda Kyando.

 

Pia ametoa wito kwa wananchi wakiona eneo linalindwa wasiingie kwa nguvu.

 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Related

ADVERTISEMENT
Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Related Posts

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE
HABARI

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI
HABARI

MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO NA WANAHABARI, JNICC
HABARI

RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO NA WANAHABARI, JNICC

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI
HABARI

MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MAKAMU WA RAIS MAREKANI ZIARANI KESHO NCHINI
HABARI

MAKAMU WA RAIS MAREKANI ZIARANI KESHO NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA
HABARI

WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In