BARUA YA ZUCHU KWA BASATA NA TCRA BAADA YA VIDEO YA MTASUBIRI KUFUNGIWA – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 16, 2022
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

BARUA YA ZUCHU KWA BASATA NA TCRA BAADA YA VIDEO YA MTASUBIRI KUFUNGIWA

SHABANI RAPWI by SHABANI RAPWI
May 7, 2022
in HABARI
0
BARUA YA ZUCHU KWA BASATA NA TCRA BAADA YA VIDEO YA MTASUBIRI KUFUNGIWA
0
SHARES
20
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

RelatedPosts

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

May 16, 2022

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E

May 16, 2022

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU

May 16, 2022
Load More

Ameandika Zuchu katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akitoa malalamiko yake kwa BASATA na TCRA baada ya video ya wimbo wa Mtasubiri sana kufungiwa.

 

BARAU YA WAZI KWA BASATA NA TCRA

Ni matumanini yangu mpaka sasa kila mtu anafahamu kua Video Ya wimbo wetu pendwa “MTASUBIRI “ Umesitishwa kuonekana kwenye vyombo vya habari Nchini kwetu .Nimeona bora nianze moja kwa moja kwenye mada husika .Jana Nilipokea taarifa hizi kupitia mitandao kama Nyinyi tu mashabiki zetu kwamba wimbo wetu unapigwa marufuku sababu tajwa kua inaleta ukakasi kwenye jamii husika mwisho wa kununukuu

Awali ya yote niseme kama msanii nilietumia ubunifu kukaa chini na muongozaji wa video yetu takribani siku 4 kuunda stori ambayo kwa utashi wangu na heshima niliyonayo kwa dini zote na madhehebu yake sikuona huu ukakasi unaoongelewa hapa.Nafahamu si kila kazi ya kisanaa itamfurahisha kila mtu lakini kuvunjia heshima dini si kitu ambacho kipo ndani ya weledi wa kazi yetu sababu tunafahamu fika tunao mashabiki wa dini zote na kulinda hisia zao ni moja ya nguzo kuu Kwenye mziki hatueki matabaka

Ifahamike kwamba mimi ndie nilishoot hiyo scene ikinitaka kuwepo kanisani nikiwa nafanya mazoezi ya kwaya sio misa ni mazoezi ya kikwaya nikiwa nimevalia joho lenye stara .Kanisa hili lipo kisarawe na kabla ya kushoot masister walitukagua na kusikiliza kwa makini stori yetu na kuridhishwa nayo ndipo hapo tukapewa ruhusa ya kushoot

Naomba nielekeze malalamiko yangu kwa mamlaka husika BASATA walezi na wazazi nimeambatanisha video na movie baadhi ambazo zimetoka kabla ya mtasubiri vipi hizi hazina ukakasi .Lakini ni jamii ipi hiyo iliyoleta malalamiko mpaka nyie kufungia video iliyogharimu muda wa siku nne na pesa nyingi kuishoot tena mkaifungia bila hata kutaka kusikiliza utetezi . Mtasubiri video ni ya kawaida sana A very innocent sweet story .Naumia sababu hii inaenda kudumaza sio tu mziki ila Tasnia nzima kwa ujumla .HAYATI baba wa taifa alisema “Utii ukizidi huzaa uoga ,Uoga huzaa unafiki na kujipendekeza mwisho wake Umauti “

Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia .Sijui nileleze vipi hisia zangu zipokelewe kwa heshima ya kutosha na utii bila ya kuchukuliwa kama mjeuri ila kwa hili mumetuonea .Sisi ni vijana tunaotafuta rizki bila ya kuchoka lakini pengine Wazazi wetu @basata.tanzania mmekua mstari wa mbele kutuvunja nguvu mbele ya jamii bila kujali hisia muda vipaji na uwekezaji unaofanyika

Hapo awali mlitoa mirabaha Wasanii wa Wcb Hatukunusa Top List Wakati kitwakwimu za namba ,MAUZO na ufanyaji vizuri Katika Chati zote Kasoro yenu nyinyi @basata.tanzania @cosotatanzania Nini shida wazazi wetu .Inawezekana vipi . Kisha hapo Tunalaumiwa kwa kutoshiriki Tuzo .

 

Ni wazi kua Hii imekua wazi sasa kama mamlaka ya kisanaa inafanya kazi Kupinga juhudi za WCB lakini pengine hii hasira mnayoipandikiza juu yetu tunaihitaji kwa mafanikio chanya yetu na mashabiki zetu wanaotupigania .mwisho niseme kazi iendelee Mashabiki zetu ,Maboss zetu mtusamahe sana kwa kero mnayokutana nayo haiko mikononi mwetu Wenye mamlaka washasema sisi ni nani? tuwe na subra na msituache mana nyinyi ndo kimbilio letu la mwisho Nawapenda sana.

Related

SHABANI RAPWI

SHABANI RAPWI

Related Posts

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE
HABARI

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E
HABARI

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU
HABARI

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
JOSE PESEIRO KOCHA MPYA WA NIGERIA
HABARI

JOSE PESEIRO KOCHA MPYA WA NIGERIA

by SHABANI RAPWI
May 16, 2022
SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI
HABARI

SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI

by I am Krantz
May 16, 2022
UKRAINE YATAKA KUUNGWA MKONO NA AFRIKA KATIKA VITA NA URUSI
HABARI

UKRAINE YATAKA KUUNGWA MKONO NA AFRIKA KATIKA VITA NA URUSI

by SHABANI RAPWI
May 16, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In