Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa aagiza kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya wilaya ya Moshi ifikapo tahe 24 Juni, 2022 kulingana na mkataba uliopo.
–
Ametoa agizo hilo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi – Kilimanjaro.
ADVERTISEMENT
–
Bashungwa amemuagiza Mkandarasi SUMA JKT kuongeza nguvu kazi na kasi ya ujenzi ili jengo hilo liweze kukamilika kwa wakati. Mradi umekadiriwa kugharimu kiasi cha Tsh Bil 2.9.
ADVERTISEMENT