Shirika la Habari la BBC kupitia mitandao yake ya kijamii wameomba radhi Kwa mashabiki wote wa Klabu ya Manchester United baada ya ujumbe uliorushwa na kituo hicho ukisomeka (Manchester United are rubbish) “Manchester United ni Takataka”
–
BBC imeeleza kuwa maandishi hayo yalitokea kimakosa kwenye habari kwa ufupi wakati wa mchuano wa Tenisi.
–
“Tunaomba radhi kwa mashabiki wowote wa Manchester United”. Mapema Jumanne ujumbe ulionekana kwenye kituo cha habari cha BBC ukisema “Manchester United ni takataka”.
–
Maandishi yalijitokeza kimakosa kwenye habari kwa ufupi chini wakati wa mchuano wa tenisi. Hii ilifuatiwa na ujumbe mwingine unaosoma “Mvua kila mahali”.
Mtangazaji Anita Mcveigh baadaye aliomba radhi kwa watazamaji, akieleza kuwa mfanyakazi ambaye alikuwa akijifunza jinsi ya kutumia mtambo huo alichapisha maandishi hayo kimakosa,