ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, May 22, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

BENKI YA CRDB KUENDELEA KUTOA MIKOPO YA WAFANYAKAZI KWA RIBA YA CHINI

I am Krantz by I am Krantz
May 4, 2022
in HABARI
0
BENKI YA CRDB KUENDELEA KUTOA MIKOPO YA WAFANYAKAZI KWA RIBA YA CHINI
0
SHARES
42
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

DSC_0507

Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiboresha maslahi ya wafanyakazi nchini pia kushusha tozo mbalimbali katika mishahara, Benki ya CRDB imepandisha kiasi cha mkopo wanachoweza kuchukua wafanyakazi pia kuongeza muda wa marejesho hadi kufikia miaka saba  ili kufanikisha shughuli zao za kiuchumi.

Kwenye maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema, benki itaendelea kutoa mikopo kwa wafanyakazi (personal loan) kwa riba ya chini ili kuwaongezea kiasi wanachoweza kukopa. Alisema benki imeshusha riba hiyo kutoka 16% hadi 12% hivyo kuongeza kiwango cha kukopa hadi Sh200 milioni kitakachorejeshwa mpaka kwa miaka saba.

RelatedPosts

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA

May 22, 2022

19 WAJERUHIWA KATIKA AJALI

May 22, 2022

MANULA AKATWA NA KIOO

May 22, 2022
Load More
DSC_0489

“Maboresho haya ni sehemu ya mkakati wa Benki ya CRDB kusaidia jitihada za Serikali kuboresha maisha ya wafanyakazi nchini,” amesema Nsekela.

ADVERTISEMENT

Maboresho mengine Nsekela amesema yamefanyika kwenye Salary Account ambayo ni akaunti maalaum kwa ajili ya wafanyakazi inawawezesha kupokea mshahara kwa urahisi. Akaunti hii imeunganishwa na huduma za kidijitali za SimBanking na Internet banking ili kumwezesha mfanyakazi kupata taarifa na kufanya miamala kwa urahisi kutoka mahali popote alipo ndani hata nje ya nchi. 

“Huduma hizi zimekuwa mkombozi mkubwa kwa wafanyakazi hususani waliopo maeneo ambako hakuna matawi yetu kwani husaidia kupata huduma zote kiganjani ikiwamo huduma ya mkopo wa kidijitali wa Salary Advance ambao hivi karibuni kiwango cha kukopa kiliongezwa hadi Sh3 milioni,” amefafanua Nsekela.DSC_0153

Kwa kushirikiana na taasisi za Serikali, Nsekela amesema Benki ya CRDB imejipanga vyema kuhakikisha mipango ya wafanyakazi inakamilishwa kwa wakati kupitia mtandao wake mpana wa huduma.

Amesema Benki ya CRDB inaongoza katika hilo kwani inao mtandao mpana wa kutolea huduma ikiwa na matawi 268 na mawakala (CRDB Wakala) zaidi ya 20,000 waliosambaa kila kona ya nchi, kuanzia mjini mpaka vijijini hivyo kuwawezesha wafanyakazi kupata huduma katika maeneo yao ya kazi hali inayowasiaidia kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za benki.

DSC_0149

Kwa wateja wanaopata matatizo ya kifamilia, Nsekela amesema Benki ya CRDB inayo Kava Assurance, huduma ya bima ya maisha ambayo imeunganishwa na akaunti ya mteja inayomwezesha kupata mkono wa pole kuanzia Sh2 milioni hadi Sh15 milioni pindi mwenza wake anapofariki au kuwafariji warithi wake yeye mwenyewe akifariki.

Benki ya CRDB kwakushirikiana na Serikali ya mkoa wa Dodoma chini ya Mkuu wa Mkoa ilifanikisha sherehe hizo kwa kuwa mzamini mkuu ikitekeleza kauli mbiu yake ya Tupo Tayari, kufanya kazi Bega kwa Bega na Serikali katika kufanikisha maendeleo ya Taifa letu. 

DSC_0474

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akifurahi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela mara baada ya kumalizika kwa sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri-Dodoma.

DSC_0265

Tawi linalo tembea(Mobile Branch) likipita mbele ya Mgeni Rasmi katika kusindikiza maadamano ya wafanyakazi.

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA
HABARI

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
19 WAJERUHIWA KATIKA AJALI
HABARI

19 WAJERUHIWA KATIKA AJALI

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
MANULA AKATWA NA KIOO
HABARI

MANULA AKATWA NA KIOO

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
NAMUNGO WAPEWA ALAMA TATU, KOCHA MAKATA AFUNGIWA MIAKA MITANO
HABARI

MAKATA, NAFTARI WAOMBA RADHI

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
VIFO MILIONI 8 KWA UVUTAJI WA SIGARA
HABARI

VIFO MILIONI 8 KWA UVUTAJI WA SIGARA

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
AMRI YATOLEWA WATANGAZAJI WANAWAKE WAFUNIKE NYUSO ZAO
HABARI

AMRI YATOLEWA WATANGAZAJI WANAWAKE WAFUNIKE NYUSO ZAO

by Shabani Rapwi
May 22, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In