ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, May 22, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki ya CRDB yaahidi neema kwa wafanyabiashara kati ya Tanzania na DRC

I am Krantz by I am Krantz
May 11, 2022
in HABARI
0
Benki ya CRDB yaahidi neema kwa wafanyabiashara kati ya Tanzania na DRC
0
SHARES
19
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO MBILI ZA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI KITAIFA DODOMA

BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO MBILI ZA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI KITAIFA DODOMA

Apr 29, 2022

Dkt. Tulia aipongeza Benki ya CRDB kuuenzi mwezi Ramadhani

Apr 20, 2022

Benki ya CRDB; Tuko tayari kufanya kazi na makampuni ya bima ya TAKAFUL

Apr 15, 2022
Load More
Benki ya CRDB imeahidi uwezeshaji mkubwa kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara kati ya Tanzania na DRC kupitia bidhaa na huduma bunifu zinazotolewa na Benki hiyo. Ahadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Congo, Jessica Nyachiro wakati wa Mkutano wa Uwekezaji na Biashara wa Tanganyika unaofanyika mkoa wa Kigoma.
Nyachiro alisema wafanyabiashara hao wakae mkao wa kula kwani Benki hiyo ipo katika hatua za mwisho za kufungua kampuni yake tanzu mjini Lubumbashi, Congo kabla ya mwisho wa mwaka huu huku akitanabaisha kuwa kuingia kwa Benki ya CRDB nchini Congo kutasaidia kurahisha biashara baina ya nchi hizi mbili.
“Ninawahakikishia wafanyabiashara wote katika Tanzania na Congo mwaka huu tutakuwa Lubumbashi,” Nyachiro alisema kwa ujasiri huku akiongezea kuwa baada ya Lubumbashi benki hiyo itaenda Kinshasa kisha Uvira na Kalemi kwani mahitaji ya huduma katika sehemu hizo ni makubwa na vilevile ni maeneo ambayo kuna biashara kubwa na Tanzania.
Congo hadi sasa ina benki 16 zikiongozwa na Rawbank na kufuatiwa na Equity Bank, hivyo kuingia kwa Benki ya CRDB kutafanya idadi ya benki nchini humo kufikia 17. Nyachiro alisema kutokana na ushindani uliopo na mazingira ya biashara ya nchini Congo mkakati wa Benki ya CRDB ni kuwekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali ya utoaji huduma ili kurahisha upatikanaji wa huduma kwa gharama nafuu na kuongeza ujumuishi wa kifedha.
Baadhi ya wafanyabiashara na wafanyabiashara wa Congo walisema wanaisubiri kwa hamu Benki ya CRDB nchini humo na wamekuwa wakitamani benki hiyo ipanue huduma zake nchini Congo muda mrefu. Meya wa Kalemi, Kakudji Kalama alisema wafanyabiashara wa pande zote mbili za Ziwa Tanganyika wanakabiliwa na changamoto nyingi za kibenki lakini ujio wa Benki ya CRDB nchini Congo utarahisisha shughuli za biashara.
“Ingawa benki itakuwa Lubumbashi, lakini ninaamini sheria na kanuni zetu zinaruhusu kupanua na kutoa huduma katika miji mikubwa. Mji wetu wa Tanganyika ndio lango la biashara nyingi za ziwa Tanganyika kutoka Tanzania…na tuna uhusiano mkubwa na Kigoma.,” Bw Kalama alisema.
Baadhi ya wafanyabiashara walisema kukosekana kwa benki kama CRDB kunawawia vigumu kuhamisha fedha kutoka Tanzania kwenda DRC hivyo kukwamisha miamala ya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.
Mfanyabiashara wa mafuta wa DRC, Bw Nondo Ibrahim, aliiomba benki hiyo kufikiria kuanza kubadilishana shilingi na faranga ili kuwaepusha na hasara na matatizo ya kubadilishana mizigo–kutoka faranga hadi dola na kisha hadi shilingi.
Kalama alisema kuwepo kwa Benki ya CRDB Congo pia kutawasaidia kutembea na fedha taslimu kwa ajili ya biashara jambo ambalo linahatarisha maisha yao na biashara kutokana na upotevu kwani kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikumbana wanyang’anyi.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Congo, Nyachiro alisema ubadilishaji wa shilingi na faranga unawezekana lakini unahitaji idhini ya Benki Kuu zote za nchi mbili. “Kwasasa tunapokea kwacha ya Zambia kwenye mpaka wa Tunduma. Hivyo tukishapata kibali inawezekana kwa faranga pia,” alisema.
Benki ya CRDB imesema mkakati wake wa kufungua ukanda wa Ziwa Tanganyika umejikita katika kuweka mazingira wezeshi yabiashara na ujasiriamali, kusaidia ujenzi wa uchumi imara wa viwanda na kuchochea ukuaji wa sekta binafsi.
Maeneo mengine ni Uwekezaji katika mifumo ya teknolojia itakayosaidia kuwezesha ukuaji wa biashara, kusaidia minyororo muhimu ya thamani ya kiuchumi na kukuza uwekezaji endelevu, pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Mbali na kukaribia kufungua kampuni tanzu nchini Congo, Nyachiro alisema Benki ya CRDB pia imeelekeza macho katika nchini za Zambia na Rwanda katika siku za usoni. Nyachiro alisema kampuni tanzu zitakazofunguliwa Lusaka na Kigali zinaendana na mpango mkakati wa benki hiyo wa kusaidia jitihada za serikali katika kukuza mahusiano ya biashara nan chi za jirani.
“Tunafanya kazi kwa karibu kwa ushirikiano na Benki Kuu za nchi hizi kuwezesha mipango yetu ya kuingia Zambia na Rwanda, alisema.
ADVERTISEMENT

Related

Tags: CRDB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA
HABARI

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
19 WAJERUHIWA KATIKA AJALI
HABARI

19 WAJERUHIWA KATIKA AJALI

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
MANULA AKATWA NA KIOO
HABARI

MANULA AKATWA NA KIOO

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
NAMUNGO WAPEWA ALAMA TATU, KOCHA MAKATA AFUNGIWA MIAKA MITANO
HABARI

MAKATA, NAFTARI WAOMBA RADHI

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
VIFO MILIONI 8 KWA UVUTAJI WA SIGARA
HABARI

VIFO MILIONI 8 KWA UVUTAJI WA SIGARA

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
AMRI YATOLEWA WATANGAZAJI WANAWAKE WAFUNIKE NYUSO ZAO
HABARI

AMRI YATOLEWA WATANGAZAJI WANAWAKE WAFUNIKE NYUSO ZAO

by Shabani Rapwi
May 22, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In