Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (Katikati), akikata utepe katika hafla ya kukabidhi vyumba vya madarasa 10 vilivyojengwa na benki ya Stanbic vyenye thamani ya TZS 159 milioni katika Kituo cha WATOTO WETU TANZANIA hivi karibuni Msata, Bagamoyo.Wengine kwenye picha ni Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo cha watoto yatima cha Watoto Wetu Tanzania,Evans Tegete (Kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Pwani – Abubakar Kunenge (wapili Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic, Kevin Wingfield (Kulia) wakishuhudia tukio hilo.Hii ni sehemu ya mpango wa Benki ya Stanbic kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha utoaji wa elimu nchini.
May, Dar es Salaam: Benki ya Stanbic Tanzania imekabidhi vyumba vya madarasa 10 vyenye thamani ya TZS milioni 159 katika kituo cha WATOTO WETU TANZANIA kilichopo Mazizi-Msata kwa kwaajli ya watoto wenye mahitaji maalumu na wanaoishi katika mazingira magumu.Hafla hiyo ilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani – Abubakar Kunenge na uongozi wa wilaya hiyo.
Msaada huo unaendana na maono ya benki ya kufanya ndoto ziwezekane huku ikikuza maendeleo ya binadamu ya Tanzania kupitia elimu jumuishi na bora. Benki imejitolea kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bora kulingana na Dira ya Maendeleo ya 2025 ya nchi.
‘Tumedhamiria kutafuta njia mpya za kufanya ndoto ziwezekane kwa wateja wetu na jamii zinazotuzunguka, na tumechagua kimakusudi kuzingatia elimu na afya kama nguzo zetu mbili kuu za kuwekeza katika maendeleo ya kijamii,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic, Kevin Wingfield.
Kwa upande wake, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete alipongeza juhudi za benki ya Stanbic za kuwekeza katika kusaidia jamii, na kuiunga mkono serikali katika azama yake ya kuleta mabadiliko endelevu kwenye sekta ya elimu kwa kuongeza upatikanaji wa elimu bora. “‘Maendeleo ya nchi yanaundwa na vitu vingi lakini jambo kubwa ni rasilimali watu ambao wana ujuzi wa kusukuma gurudumu hilo, inabidi tuhakikishe vijana wetu wanapata elimu bora ambayo itawawezesha kubuni mbinu mbadala za kutatua changamoto za jamii, vile vile kushindana katika soko la ajira duniani.” alisema.
Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Pwani – Abubakar Kunenge alisema Kupitia uchangiaji huu wa vyumba vya madarasa, Stanbic imesaidia kwa kiasi kikubwa kujenga wataalamu watakao jenga taaifa la kesho
Madarasa hayo 10 pia yatatumiwa na wasichana waliokatisha masomo kutokana na mimba za utotoni.
Kama sehemu ya uwekezaji katika jamii, Stanbic imetoa zaidi ya TZS bilioni 1 kusaidia sekta ya elimu ya Tanzania; kwa kujenga vyumba vya madarasa, kuchangia madawati, na kukarabati miundombinu ya shule kama vile vyoo ili kuboresha usafi wa mazingira katika shule mbalimbali.