Rais Joe Biden wa Marekani ametoa wito wa kufanyika kwa mabadiliko ya sheria ya umiliki wa silaha nchini humo baada ya kijana mmoja kuwauwa wanafunzi 19 kwenye shule moja ya msingi katika jimboni Texas.
–
Akizungumzia tukio hilo Biden amesema inashangaza sana kuwa mpaka leo Marekani inashindwa kupingana na kundi la wanaopigania umiliki holela wa silaha, licha ya kujua kwamba kila siku watu wasio hatia wanauawa.
ADVERTISEMENT
–
Biden, ambaye mwenyewe amewahi kuondokewa na watoto wake wawili, amesema hajui kinachowafanya Wamarekani kushindwa hadi leo kuchukuwa hatua dhidi ya hali hiyo.
ADVERTISEMENT