Waziri wa Nishati, January Makamba amesema, Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 100 kama ruzuku kwenye mafuta ili kuleta nafuu ya bei ya mafuta kuanzia Juni Mosi, 2022 katika kipindi hiki cha mpito kuelekea mwaka mpya wa fedha.
–
Akiwasilisha taarifa ya serikali bungeni, Waziri wa Nishati, January Makamba amesema ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2021/22. Kutolewa kwa ruzuku hii hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea.
–
“Rais Samia Suluhu ametoa maelekezo kwamba, katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane na ijinyime na zitolewe shilingi bilioni mia moja kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini.”
–
“Ruzuku hii (Shilingi Bilioni 100) inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2021/22. Kutolewa kwa ruzuku hii hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea.” amesema Makamba