BIMA YA KILIMO YA BENKI YA NMB YAMKOMBOA MKULIMA – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 16, 2022
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

BIMA YA KILIMO YA BENKI YA NMB YAMKOMBOA MKULIMA

I am Krantz by I am Krantz
May 12, 2022
in HABARI
0
BIMA YA KILIMO YA BENKI YA NMB YAMKOMBOA MKULIMA
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

Tunafahamu kilimo chetu Watanzania kinategemea hali ya hewa, hivyo hasara ya kutokupata mazao inaweza kutokea. Ikishirikiana na makampuni ya bima, Benki ya NMB inamlinda mkulima dhidi ya hasara ya itakayotokana na mvua ya mawe, moto, ukame, mvua nyingi, uharibifu wa baridi, mafuriko na radi.

Kwa mujibu wa NMB, bima hii inahusisha mazao yote ya biashara ikiwemo; Ngano, mahindi, shayiri, mpunga, chai, kahawa, miwa, tumbaku, mazao yote ya mbogamboga, maua na mazao ya miti.

RelatedPosts

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

May 16, 2022

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E

May 16, 2022

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU

May 16, 2022
Load More

Pia, unaweza kununua bima hii kwa ajili ya mali na vifaa vya kilimo pamoja na mazao yaliyovunwa, shamba kitalu na vifaa vya umwagiliaji.

Vile vile, bima hii inategemea na thamani ya pembejeo au bei ya soko iliyokubaliwa mapema ya mazao yaliyopandwa.

Faida ukiwa umebima shamba lako kupitia Benki ya NMB;

  • Utapata mikopo ya kilimo kwani hati ya sera ya mazao inakubaliwa na taasisi za kufadhili kama njia mbadala ya dhamana
  • Kujikinga dhidi ya hasara kwa kupewa kiinua mgongo kipindi cha msimu mbaya wa mazao
  • Elimu ya biashara ya kilimo kupitia wataalamu wetu katika sekta hio.

Bima hii ya mazao ni uvumbuzi wa kifedha ambao huchochea uwekezaji katika sekta ya kilimo kupitia kuongezeka kwa ufikiaji wa fedha na motisha kwa wadau wote.

Kisichokingwa na bima hii ni hasara yoyote ya mazao itokanayo na majanga ambayo hajakatiwa bima, kupungua kwa mazao na kupungua ubora kwasababu ya usumbufu au ajali katika mchakato mzima wa kazi.

Pia, hasara itokanayo na ucheleweshwaji uvunaji, kukamatwa au kushikiliwa, kuzuia mazao au vifaa, makosa katika matumizi ya dawa kwa kushindwa kufuata mapendekezo juu ya taratibu za matumizi, wizi, upotevu usieleweka na hasara isiyohesabika.

Kiwango cha bima kinategemea aina ya mazao, eneo, ukubwa wa shamba na  idadi ya vihatarishi. Kiwango hiki ni kati ya asilimia 4.5 na 6 kwa ujumla inayokatiwa bima.

Unachohitaji ni;

  • Fomu ya maombi iliyojazwa kikamilifu na malipo ya bima
  • Ripoti ya mazao kupandwa iliyoandaliwa na mtoa bima
  • Muafaka wa madai
  • Hasara ya mazao/uzalishaji

Malipo yote ya madai yatafanyika mwisho wa msimu wa mazao, hata hivyo inapotokea hasara kubwa inayohitaji kuotesha mazao upya basi malipo yatafanyika kuwezesha kuotesha mazao upya.

Tembelea tawi lolote la benki ya NMB lililopo karibu yako kujipatia bima hii.

Umebima-SiNgumuKihivyo!

 

Related

I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE
HABARI

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E
HABARI

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU
HABARI

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
JOSE PESEIRO KOCHA MPYA WA NIGERIA
HABARI

JOSE PESEIRO KOCHA MPYA WA NIGERIA

by SHABANI RAPWI
May 16, 2022
SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI
HABARI

SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI

by I am Krantz
May 16, 2022
UKRAINE YATAKA KUUNGWA MKONO NA AFRIKA KATIKA VITA NA URUSI
HABARI

UKRAINE YATAKA KUUNGWA MKONO NA AFRIKA KATIKA VITA NA URUSI

by SHABANI RAPWI
May 16, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In