Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha tarehe 16 Mei,2022 amepokea ujumbe kutoka Shirikisho la Dunia la mchezo wa Baseball and Softball (WBSC) ambaye ni Mratibu wa Shirikisho hilo Afrika ndugu Mattia Berardi.
Berardi amefika Ofisi za BMT kujitambulisha lakini pia amefika nchini kuona maandalizi ya mashindano ya Afrika baseball 5 kufuzu kombe la dunia yanayotarajiwa kutimua vumbi kuanzia tarehe 23 – 26 Mei, 2022 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Ujumbe huo uliambatana na Viongozi wa kamati ya Utendaji ya chama cha mchezo huo cha taifa ukiongozo na Katibu Mkuu Alpherio Nchimbi.