Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema John Mrema amethibitisha kuwa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, anatarajiwa kuwa mgeni maalumu katika kikao cha Baraza Kuu la Chadema litakalofanyika Jumatano Mei 11.
–
Mrema amesema jana Mei 9, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kikao hicho, kitakachotanguliwa na kikao cha kamati kuu itakayoketi kesho Jumanne Mei 10, 2022.
–
Chadema kitafanya kikao cha baraza kuu litakalokuwa ajenda tano na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho, watakaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar.
–
Bobi Wine aligombea urais wa Uganda kwa tiketi ya chama cha National Unity (NUP),Platform katika uchaguzi uliopita.