Ameandika Omarr Kombo :
Ukitaka kujua utukufu wa Mwenyezi Mungu usitazame chini nyanyua kichwa chako juu utazame anga,nyota, mwezi na jua hakika kuna jambo la kushangaza utalijua kuhusu nguvu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
–
Ukitaka kujua Jonh Bocco ni mshambuliaji hatari na anayestahili heshima katika historia ya soka hapa nchini ,basi inabidi uvue kofia ya uyanga na Usimba na fikra zako ziende mbali kwenye ulimwengu wa mawazo, ulimwengu ambao unaongozwa na mantiki kuliko hisia, ulimwengu unaongozwa na sayansi kuliko imani.
–
Basi tumpe Mwenyezi Mungu sifa na utukufu wake kwasababu kila kilichopo kwenye ulimwengu huu ni mali yake,na tukumbuke ile kazi kubwa inayofanywa na miguu ya Jonh Bocco inastahili pia sifa na utukufu na zaidi tukayakatae yale mafundisho ya nabii hakubaliki kwao.