Uongozi wa Ligi Kuu England umethibitisha kuuzwa kwa klabu ya Chelsea kwenda kwa mmiliki mwenza wa timu ya baseball ya Marekani LA Dodgers Todd Boehly, umiliki wenye thamani ya bilioni 4.25.
–
Uongozi huo umesema baada ya kupitia kwenye majaribio mbalimbali kuwa sasa wamiliki hao wamepata baraka za uongozi wa Ligi na wanaweza kuendelea kuwekeza.
–
Klabu ya Chelsea iliwekwa sokoni baada ya Urusi kuivamia Ukraine kutokana na kile kilichoelezwa kuwa bilionea Roman Abramovich anaushirika na Rais wa Urusi Vladmir Putin.
–
Baada ya EPL kupitisha sasa imebakia nafasi ya serikali kupitisha uuzaji huo ambapo unatakiwa kukamilizika kabla ya Mei 31.