BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inatangaza kuwa muda wa kuanza kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Na. 208 katiya Dodoma Jiji FC na Young Africans SC ni saa 10:00 jioni badala ya saa 1:00 usiku kama ilivyokuwa awali.
–
Mchezo huo utachezwa Mei 15, 2022 kwenye uwanja wa Jamhuri uliopo jijini Dodoma kama ilivyoainishwa kwenye ratiba ya Ligi.
–
Sababu ya mabadiliko hayo ni uwanja wa Jamhuri kuwa na matumizi mengine kuanzia asubuhi ya Mei 16, 2022 hali inayolazimu maandalizi ya shughuli hiyo yafanyike na kukamilika usiku wa Mei 15, 2022.
ADVERTISEMENT