Mwenyekiti wa zamani Simba, Ismail Aden Rage amemtaka Mwekezaji wa Klabu hiyo Mohamed Dewji (Mo) kuivunjilia mbali Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo kwani imejaa wababaishaji.
–
Rage akizungumza leo siku moja baada ya kauli ya Mwekezaji huyo kusema kuwa kuna haja ya kuifumua timu yao nzima na kuisuka upya, ametaka hilo lifanyike kwanza kwa kuivunja Bodi hiyo ya Wakurugenzi kwani haina watu wa kweli wa mpira bali wanamdanganya tu.
–
Rage amesema haoni pia sababu ya kocha wa Pablo Franco kutimuliwa bali kwanza waanzie kwenye bodi ya Klabu hiyo.
–
Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na Yanga jana katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Azam huko Mwanza na kuvuliwa ubingwa wa Kombe hilo.