Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema kwamba wiki ijayo watakutana na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kufanya kikao cha pamoja chenye lengo la kujadili mambo ya msingi ya kujenga taifa pamoja na kutengeneza mahusiano mazuri ya vyema hivyo.
–
Mbowe ameyasema hayo leo Mei 11, 2022 wakati akizungumza kwenye Baraza Kuu la Chama hicho, Dar es Salaam.
–
“Juzi wakati tunajiandaa na Baraza Kuu, Rais Samia aliomba tuonane tena nikaenda kumuona tulikuwa na kikao cha masaa mawili, tumekubalina kwamba kutakuwa na kikao kingine Wiki ijayo kati ya Rais Samia na ujumbe wake wa Viongozi wa Serikali na CCM na Viongozi wasiozidi 10 wa CHADEMA wakiongozwa na Mimi, tutakwenda kuzungumza ni nini kinafanya tunashindwa kuelewana katika kulipeleka Taifa letu mbele”
–
“Wiki ijayo tutaanza vikao vya CHADEMA na Rais na CCM na Serikali yake, tuulizane mambo ya msingi tukitambua kuwa sisi tukiweza kujenga mahusino ya msingi wenzetu nao watajiunga na sisi kutengeneza mahusiano mazuri”
–
“Watu wetu wamekuwa na hofu kwasababu ya kutoamiana, hata ukienda kwenye Mataifa ambayo yamepigana vita kwa miaka mingi, yamefanyiana ubaguzi kama Afrika Kusini wakati Mandela yupo Jela alikuwa anaendelea kufanya mazungumzo na Watawala, Makaburu wa Afrika Kusini”
–
“Wana CHADEMA hatuwezi kuponya matatizo ya Taifa letu pekee yetu tunayaponya kwa kuangalia CCM, ACT, CHAUMMA, Vyama vingine na waisokuaa na Vyama ili tulilete Taifa letu pamoja”
–
“Nilimwambia Rais wakati wa Katiba bora na mpya ni sasa na nimemuhakikishia CHADEMA hatutaacha ajenda yetu ya Katiba Mpya na pia nilimuuliza Mama kwanini mnaogopap katiba?” .