Korea Kaskazini imeripoti vifo vya watu 21 kutokana na tatizo la Uviko-19 ambalo limeingia nchini humo ikiwa ni siku ya pili tu.
–
Rais wa nchi hiyo Kim Jong Un ameliita tukio hilo kama janga kubwa katika historia ya nchi hiyo na kuzitaka mamlaka husika, Serikali pamoja na wananchi kuungana kwa pamoja na kupambana kuhakikisha janga hilo linakwisha haraka.
Jumla ya wagonjwa wapya 174,440 wamegundulika kuwa na hali ya homa ambapo kwa siku ya jumamosi pekee Serikali ilithibitisha jumla ya watu 27 kufariki dunia na wengine 524,440 walilazwa kutokana na virusi hivyo.
–
Hadi sasa jumla ya watu 280,810 wapo karantini kutokana na kuambukizwa vizrusi hivyo, Rais Kim aliitisha kikao cha dharura kujadili njia za kukabiliana na tatizo hilo na kuchukua hatua za haraka za kumaliza kabisa tatizo hilo.
–
Chombo cha Habari cha Serikali kiliripoti kuwa vipimo vya sampuli kutoka kwa watu mbalimbali vilichukuliwa na kupelekwa Pyongyang na baada ya uchunguzi kufanyika ikathibitika kuwa watu walikuwa wameathiriwa na kirusi aina ya Omicron.