Mamlaka ya hifadhi ya Mikumi Morogoro imesema Dereva ambaye alimgonga tembo na kumuua wiki mbili zilizopita wakati akipita ndani ya hifadhi hiyo amelipishwa faini ya $ 15000 ambazo ni zaidi ya milioni 34.
–
Herman Baltazary ambaye ni Kaimu Mkuu wa Hifadhi hii ambayo ndani yake kunapita barabara kuu kwenda Mikoa mbalimbali ameiambia Ayo TV kwamba sio tembo peke yake aliyegongwa toka mwaka 2022 umeanza kwani kuna nyati wawili waligongwa na kufa huku Dereva aliyewagonga pia akifariki.
–
Mbali na faini ya dola 15000 anayotozwa Mtu aliyemgonga Tembo, Herman amesema faini ya kumgonga Nyati mmoja ni dola 2500 ambayo ni Tsh. milioni tano, laki nane na elfu kumi na nne.