ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, March 22, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

DK. MPANGO AMFUNDA BALOZI POLEPOLE WAKIZUNGUMZA JIJINI DODOMA, JANA

Ally Hamis Zingizi by Ally Hamis Zingizi
May 6, 2022
in HABARI
0
DK. MPANGO AMFUNDA BALOZI POLEPOLE WAKIZUNGUMZA JIJINI DODOMA, JANA
0
SHARES
184
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

Mar 21, 2023

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

Mar 21, 2023

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

Mar 21, 2023
Load More

Makamu Dk. Philip Mpango jana alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi anayekwenda kuiwakilisha Tanzania Nchini Malawi Balozi Humphrey  Polepole,  Ofisini kwake, jijini Dodoma.

Makamu wa Rais amempongeza kwa  kuteuliwa na imani aliopewa katika kuliwakilisha taifa nchini Malawi na kumsihi kwenda kufanya kazi kwa weledi na uzalendo kwa maslahi ya taifa.

Makamu wa Rais amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo mkubwa katika kutekeleza diplomasia ya uchumi hivyo amemtaka Balozi Polepole kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi utakaokuwa na manufaa kwa Tanzania.

Amesema nchi za Afrika zina uwezo wa kufanya uwekezaji baina ya mataifa yao na kupata manufaa makubwa hivyo amemsihi Balozi Polepole kuvutia wawekezaji wa Malawi hapa nchini pamoja na kutafuta fursa za uwekezaji nchini Malawi.

Aidha amemuasa kutambua vipaumbele vya taifa ikiwa ni pamoja na kufahamu takwimu za msingi zilizopo katika Dira ya taifa na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano pamoja na vipaumbele vilivyopo katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020,  zitakazochagiza katika kutafuta wawekezaji.

Halikadhalika amemuagiza Balozi Polepole  kuhakikisha anashiriki katika mikutano mbalimbali itakayowezesha kujifunza,  kueleza mazuri ya Tanzania pamoja kuvutia wawekezaji. Amesema ni muhimu kuendelea kuitangaza lugha ya Kiswahili katika nchi hiyo ikiwemo kutafuta fursa ya kufundishwa kwa lugha hiyo nchini Malawi.

Aidha amemuasa kuwaunganisha watanzania wanaoishi nchini Malawi  ili kuwa na mawazo ya pamoja namna wanavyoweza kuwekeza hapa nchini na kurudisha ujuzi na maarifa walioyonayo nyumbani Tanzania.

Makamu wa Rais amemsihi Balozi Polepole kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha zinazopelekwa katika kuendesha ubalozi huo  ili kuongeza tija ya uwakilishi nchini humo.

Kwa upande wake Balozi Humphrey Polepole amemshukuru Makamu wa Rais kwa miongozo aliompa na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya taifa la Tanzania. Amesema tayari ameanza kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo zinazoweza kutatuliwa kupitia mamlaka za Tanzania kama vile Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
Ally Hamis Zingizi

Ally Hamis Zingizi

Related Posts

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI
HABARI

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA
HABARI

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI
HABARI

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
BIKIRA JANE APATA MTOTO
HABARI

BIKIRA JANE APATA MTOTO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA
HABARI

ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA

by ALFRED MTEWELE
Mar 21, 2023
SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO
HABARI

SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In