Muinjilisti mmoja ameingia mashakani baada ya kuwaambia watu kuwa anajua lango linaloelekea mbinguni lililopo eneo la kusini -magharibi mwa Nigeria ambalo anaweza kuwaonyesha -kwa malipo.
–
Mchungaji Ade Abraham aliripotiwa kwa polisi na mmoja wa wafuasi wake, ambaye alisema mchungaji huyo alimtoza naira 310,000 (sawa na $750; £600) kulitazama eneo linakopatikana lango hilo katika mji wa Araromi-Ugbeshi, uliopo katika jimbo la Ekiti.
–
Kiongozi huyo wa kidini alikiri kwamba alikuwa ametoa kauli kuhusu lango la mbinguni, akisema kuwa ni “Mungu anayemtumikia ” ambaye alimfunulia ili kuijaribu imani ya watu wa kanisa lake, lakini hakujapokea malipo yoyote.
–
Jumuiya ya Wakristo wa Nigeria imetoa taarifa ya kumkana Mchungaji Ade Abraham, na polisi ya jimbo la Ekiti imekusanya taarifa za maandishi kutoka kwa wafuasi wa kanisa lake na kuanzisha uchunguzi.
Chanzo – bbcswahili