Kampuni ya EA Sports imethibitisha kujitoa kwenye ushirikiano wa takribani miaka 30 na FIFA, hivyo kutoendelea na utengenezaji wa gemu za video chini ya jina la FIFA.
–
FIFA 23 ndio itakuwa toleo la mwisho la mfululizo wa gemu hiyo maarufu ya video.
EA wataendelea kutengeneza gemu hizo za soka lakini kwa kutumia jina jipya la EA Sports FC.
–
Gharama za leseni ya kuchapisha gemu hizo ndio sababu kubwa iliyopelekea EA kufikia uamuzi huo.
Wakati huohuo bosi wa FIFA Gianni Infantino ametangaza mipango yao ya kutengeneza gemu zao wenyewe za video.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT