ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Kocha wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amethibitisha kuwa watakosa huduma ya kiungo Fabinho katika mechi ya fainali za kombe la FA dhidi ya Chelsea Jumamosi ijayo.
–
Fabinho alipatwa na jeraha katika mechi iliyochezwa Jumanne dhidi ya Aston Villa.
–
Kiungo huyo pia hatocheza katika mechi mbili za mwisho za Ligi katika msimu, hata hivyo Klopp amesema kuwa ana matumaini kuwa Fabinho atakuwa fiti kucheza katika fainali za Ligi ya Mabingwa mnamo Mei 28, 2022.