FILAMU YA THE ROYAL TOUR HAINA MAANA TUKISHINDWA KUHIFADHI NA KULINDA VIVUTIO VYA UTALII – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, May 19, 2022
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

FILAMU YA THE ROYAL TOUR HAINA MAANA TUKISHINDWA KUHIFADHI NA KULINDA VIVUTIO VYA UTALII

Ally Hamis Zingizi by Ally Hamis Zingizi
May 14, 2022
in HABARI
0
FILAMU YA THE ROYAL TOUR HAINA MAANA TUKISHINDWA KUHIFADHI NA KULINDA VIVUTIO VYA UTALII
0
SHARES
49
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

May 19, 2022

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

May 19, 2022

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

May 19, 2022
Load More

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akizungumza na Maafisa na Askari wa Uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi ambapo amewataka kuhakikisha wanalinda vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuleta maana ya uwepo wa   Filamu maarufu ya ‘The Royal Tour’ 

Baadhi ya Maafisa na Askari wa Uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi wakiwa wamesimama kikakamavu  kwa ajili ya kukaguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi mara baada ya kuwasili katika kituo cha mafunzo ya Kijeshi cha Mlele kilichopo mkoani Katavi kwa ajili ya kufunga mafunzo hayo

Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Filberto Sanga ( wa pili kushoto) akizungumza na Mratibu wa Jeshi la Uhifadhi, Fidelis Kapalata  mara baada ya Naibu Waziri hiyo kufunga mafunzo ya Kijeshi kwa Wahitimu 190 kutoka TANAPA,  TAWA, NCAA na TFS, Wengine ni Wqjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi

Baadhi Maaafisa na Askari wa Uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi wakipita mbele ya Jukwaa kuu kwa Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi ambapo amewataka Wahitimu hao kuwa mfano kwa jamii kwa kutanguliza mbele uzalendo ili kulinda maliaasili za wanyamapori, misitu ba mazao yake.

Mratibu wa Jeshi la Uhifadhi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Fidelis Kapalata akizungumza mbele ya Mgeni rasmi wa kufunga mafunzo kwa wahitimu 190 ambao ni Maafisa na Askari wa Jeshi la Uhifadhi nchini ambapo amesema Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Mlele kinakabiliwa na changamoto ta ubovu wa muungano hivyo Wizara iweze kusaidia ili kuondokana ha na adha hiyo

Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi  akikagua gwaride  huku akiwa ameongozana naAskari wa Jeshi la uhifadhi Bw.Fahari Makombe wakati akikagua gwaride la Wahitimu 190 ambao ni Maafisa na Askari wa Jeshi la Uhifadhi nchini katika Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Mlele kilichopo mkoani Katavi

Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi ( katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Filberto Sanga ( wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya  Wahitimu 190 ambao ni Maafisa na Askari wa Jeshi la Uhifadhi nchini katika Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Mlele kilichopo mkoani Katavi

……………………………………………..

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi amewataka  Maafisa na Askari wa Uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi kuhakikisha wanalinda vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kuongeza kuwa Filamu maarufu ya ‘The Royal Tour’ iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan haitakuwa na maana kama vivutio hivyo havitalindwa

Naibu Katibu Mkomi  ameyasema hayo Ijumaa Mei 13, 2022 alipokuwa akifunga mafunzo ya kijeshi kwa Maafisa na  Askari 190 kutoka TFS, TANAPA, NCAA na TAWA katika kambi ya mafunzo ya kijeshi Mlele mkoani Katavi.

” Filamu ile imezinduliwa  kwa lengo la kuhamasisha shughuli za utalii na Uwekezaji nchini na tangu izinduliwe kila Mtanzania na Dunia wanafahamu  Tanzania kuna nini” amesema Naibu Katibu mkuu huyo.

Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, tangu filamu hiyo izunduliwe inafanya vizuri Kimataifa na tayari Marekani  imeoneshwa katika vituo 300 kati ya vituo 355 vilivyoripotiwa kuonesha filamu hiyo.

Amesema mafunzo hayo yakawe chachu ya kuimarisha sekta ya utalii na  kuhakikisha Watalii wanapata huduma katika mazingira bora ili kuendana na maono ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amewaeleza  Wahitimu hao kuwa  wana wajibu wa kulinda misitu, wanyamapori, malikale na vyote ambavyo vinawavutia watalii kuja kutembelea.

” Niwaombe Wahitimu mkatanguliza mbele uzalendo kwa kuhifadhi na kulinda vivutio vyote vya utalii vitakavyokuwa chini yenu, msipotoa huduma nzuri kwa watalii Filamu ya Royal Tour haitakuwa na maana yoyote” amesisitiza Naibu Katibu Mkuu.

Kwa upande wake Mratibu wa Jeshi la Uhifadhi, Fidelis Kapalata amesema mafunzo hayo waliyoyapata katika yanakwenda kubadili mfumo wao kufanya kazi hususan katika kipindi hiki ambacho ujio wa watalii utakuwa mkubwa kufuatia kuzinduliwa kwa Filamu maarufu ya Royal Tour

Mwakilishi wa Kamishna wa Uhifadhi – TFS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia – Utawala (SACC-Admn), Luoga Erasto anasema ni matarajio ya Jeshi la Uhifadhi – TFS baada ya mafunzo hayo wahitimu watakwenda kuishi utamaduni wa kijeshi na kuongeza kasi, ufanisi na uzalendo katika utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi wa rasilimali za nchi.

“Niipongeze Wizaya ya Maliasili na Utalii kwa kuratibu mafunzo haya yenye lengo la kubadirisha mfumo wa utendaji toka ule wa kiraia na kuwa wakijeshi, sasa taasisi zote za Wizara zinakuwa na mfumo mmoja wa kijeshi ambao utasaidia katika mabadiliko ya kiutendaji,” anasema SACC Luoga.

Katika mahafali hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Filberto Sanga aliomba Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia uwezekano wa kuwapangia kazi wilani mwake baadhi ya wahitimu kutoka kila taasisi ya uhifadhi ili waweze kulinda maliasili zilizopo mkoani Katavi kwa kile alichodai mkoa huo umebarikiwa vivutio vingi vya utalii na vingi vikiwa wilayani Mlele.

Related

ADVERTISEMENT
Ally Hamis Zingizi

Ally Hamis Zingizi

Related Posts

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA
BIASHARA

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU
HABARI

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

by I am Krantz
May 19, 2022
“PANYA ROAD” KAENI CHONJO SERIKALI IPO KAZINI
HABARI

“PANYA ROAD” KAENI CHONJO SERIKALI IPO KAZINI

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
RAIS SAMIA AMETOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU-MAJALIWA
HABARI

RAIS SAMIA AMETOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU-MAJALIWA

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO
BIASHARA

WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
TUMEUMIZWA NA MATOKEO YA JANA – AHMED ALLY
HABARI

TUMEUMIZWA NA MATOKEO YA JANA – AHMED ALLY

by Shabani Rapwi
May 19, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In