Mshambuliaji wa klabu ya Asante Kotoko ya Ghana, Franck Mbella ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon kwaajili ya mechi za kufuzu AFCON 2023.
–
Mbella mwenye umri wa miaka 22 ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya Ghana hadi sasa akiwa amefunga mabao 19 katika 24 alizocheza pamoja na kutoa pasi za mabao mbili.
–
Nyota huyo amekuwa akihusishwa kutakiwa na vilabu kadhaa ikiwepo klabu ya Simba SC, Sevilla, Atletico Madrid na Elche.