Wauzaji wa bidhaa wakubwa na wakati hapa nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya jukwaa la kidigitali linalokuwa kwa kasi na lenye watumiaji wengi, kwa ajili ya kuuza bidhaa zao kwa urahisi na mazingira rafiki kwa wanunuzi.
–
Jukwaa hilo mtandao lililowekwa katika mfumo wa programu tumizi (App) linajulikana kama Tunzaa na linapatikana kwenye simu janja.
Kampuni ya Tunzaa Fintech iliyobuni programu hiyo imesema tangu kuanza kwake, muitikio wa wateja mtandao umekuwa mkubwa na kufanya bidhaa kuadimika na hivyo kutoa wito kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo ili kuuza bidhaa zao kukidhi mahitaji ya wateja hao.
–
“App yetu ya Tunzaa inawawezesha watumiaji wake kulipia fedha kidogo kidogo wanaponunua bidhaa kama vyombo vya nyumbani, vifaa vya umeme au kufanya safari za kitalii kwa wakati husika. Mnunuzi anapokamilisha malipo, basi anapata bidhaa yake au huduma anayoihitaji kwa wakati husika.” amesema Mkurugenzi na Muanzilishi wa Tunzaa, Ng’winula Kingamkono.
–
Hadi sasa wauzaji zaidi ya 30 wanatumia mfumo huo na kuna bidhaa Zaidi ya 1400 zinazopatikana kwenye App hiyo.