Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael Mgombela amefariki dunia baada ya gari alilokua anaendesha
Toyota Hilux lenye namba za usajili T 840 DQF kugonga kiberenge cha treni chenye namba za usajili HDTC4 mali ya Shirika la Reli katika makutano ya barabara na reli eneo la Kilimahewa Manispaa ya Morogoro.
–
RPC wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo May 23,202 na kwamba kiberege hicho kilikua kinatokea Kilosa kuelekea Morogoro mjini.
–
Kamanda Musilimu amesema katika ajali hiyo amepatikana pia majeruhi mmoja Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Razia Kassimu ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro.