Mwanamuziki Hamisi Baba aka H.Baba ameibuka kudai haki yake kutoka kwa mwanamuziki mwenzake Harmonize ambae wamewahi kufanya nae kazi ya ushirikiano kupitia wimbo wa “Attitude” ambao ulitoka Aprili 23, mwaka jana akiwemo pia gwiji kutokea DR Congo, Awilo Longomba.
–
Kupitia ukurasa wake wa instagram, H.Baba amedai kudhulumiwa jasho lake (haki) kutokana na ushiriki wake katika wimbo huo kwa kutoambulia chochote katika pande zote mbili yaani audio na video na kusihi kwamba Harmonize amlipe.
–
“Nakuheshimu sana, usidhulumu jasho langu mdogo wangu” inasomeka sehemu ya ujumbe wa H.Baba aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram. Wimbo “Attitude” ni moja kati nyimbo kutoka kwa Harmonize iliyopata mafanikio makubwa, hadi sasa video ya wimbo huo ina views Milioni 15 katika mtandao wa youtube huku Boomplay ukiwa na streams Milioni 2.1