Msanii Harmonize amemnunulia mama yake zawadi ya gari jingine aina ya ‘Toyota Harrier’ baada ya kurejea kutoka nchini Kenya alikoenda kwenye shoo za kimuziki.
–
Kupitia Insta-story ya akaunti yake ya Instagram, Harmonize ameandika:
“Mama Kondeboy hakuna gari anayoipenda zaidi ya Harrier usikute enzi za ujana wake kuna mtu alimtesa kisa gari hii!
“Ndo maana hataki gari ya aina nyingine, haya mama here we go mwanao nimerudi kutoka Kenya mihangaikoni changamoto za hapa na pale mara kuitwa polisi na kurushiwa maji kwa makosa ya watu wenye tamaa ila finally sikurudi mikono mitupu, nimekuongezea hii nyingine mama Kondeboy!”
Hii ni mara ya pili Harmonize kumnunulia mama yake gari baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 2019.