Mtangazaji wa Wasafi FM Diva The Bawse amesema kuwa pamoja na kuwa ameolewa na Sheikh Abdullahzack ila yeye havai ushungi na hata mumewe anajua hilo na ndo maana hamuingilii kwenye ushungi.
–
“Nguo nimebadilisha. Sivai sana nguo fupi. Lakini kichwa sivai maushungi, mtanisamehe mimi ni Diva hizo vishungi sivai.Hata Abdul anajua, labda kama tunaenda msikitini Ijumaa ndiyo nitavaa. Kuna zile sehemu ambazo nikienda nitavaa, lakini nikienda ofisini mimi ni Diva yule yule”