Bi. Anna Qabale Duba (31) ambaye ni muuguzi kutokea kaunti ya Marsabit nchini Kenya ametunukiwa tuzo ya muuguzi bora duniani kwa kampeni yake ya kupinga ndoa za utotoni na ukeketwaji wa wanawake.
–
Tuzo hiyo ijulikanayo kama Aster Guardians Global Nursing kutokea Dubai ina thamani ya dola za kimarekani 250,000 na ilikuwa inashindaniwa na wauguzi 24,000 ambao majina yao yalipendekezwa.
–
Anna ndiye msichana pekee mwenye shahada ya Chuo Kikuu kutokea kijijini kwao pia ndio msichana pekee aliyesoma zaidi ya elimu ya msingi katika familia yao yenye watoto 19.
Alikeketwa akiwa na umri wa miaka 12 na alinusurika ndoa ya kulazimishwa akiwa na umri wa miaka 14.
–
Shule anayoiendesha hufundisha mambo ya msingi ikiwemo kusoma na kuandika ambapo watoto hupata mafunzo asubuhi na baadaye ni zamu ya wazazi. Vilevile wazazi hufundishwa mambo ya msingi kuhusu elimu ya afya ya uzazi n.k
–
Akihojiwa na kituo cha habari cha BBC muuguzi huyo amesema kuwa ”tuzo hii itanisaidia kupanua shule yangu ili isambae katika nchi nzima ya Kenya”.