Mkoa wa Iringa unatarajia kutoa chanjo ya polio kwa watoto laki moja na elfu 68 na 658 walio na umri wa chini ya miaka mitano.
–
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya polio katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa, Mganga Mkuu wa mkoa huo Dkt. Mohamed Manguna amesema, chanjo hiyo itatolewa kwenye vituo 598.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amewataka wananchi wa mkoa huo kuacha imani potofu juu ya chanjo hizo ili kuwalinda watoto dhidi ya polio.
–
Ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo na kuwaomba viongozi wa dini kushirikiana na serikali kuwashawishi wazazi ili wawapeleke watoto wao kupata chanjo. Serikali ilitangaza kampeni ya chanjo dhidi ya polio baada ya kuripotiwa kuwepo na maambukizi ya ugonjwa huo nchini Malawi. Ugonjwa wa Polio unasababisha mtoto kupooza, kupata ulemavu wa kudumu na hata kufariki dunia.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT